Binti huyu nae aangaliwe!
Hili bado linawaumiza wanawake wengi hususani walio vijijina hasa katika zama hizi za Ari,nguvu na kasi mpya ambayo inatakiwa kumpa maisha bora kila mtanzania.
Nazungumzia suala la wanafunzi waliozaa kutokubaliwa kurudishwa mashuleni, ikiwa Elimu ndio msingi mkubwa wa maisha na ndio njia mojawapo ya kujiletea maendeleo je bila hiyo elimu binti huyu atawezana kweli na kasi hii.
Wengi wamekuwa wakilitazama hili kwa upande mmoja tu,aidha bado jambo hili wanalisikia toka kwa mtu mwingine na sio kwamba limeshamfika yeye mwenyewe au ndugu yake.
Katika kukuza kiwango cha elimu mambo mengi yalifanyika ikiwa ni pamoja na kufuta ada za mashuleni kwa kuwa kila mtu ana haki ya kupata elimu ili aweze kuyamudu maisha,serikali ingemuangalia binti huyu na kumuweka katika kundi hilo la wenye haki hiyo.
Safari bado ni ndefu katika ukombozi wa mwanamke ila ninaamini kama kila mtu atayaona matatizo ya mwanamke mwenzie kuwa ni yake tutaweza kufika huko ambako tunapataka.Hasa kwa kutumia muhimili wetu wa Bunge kupitia wawakilishi wetu ambao siku zinavyozidi kwenda wanakuwa wengi bungeni na katika nyadhifa mbalimbali.
Nawatakia kila lakheri!